,

Elimu Quotes

Quotes tagged as "elimu" Showing 1-15 of 15
Enock Maregesi
“Ukitaka kufanikiwa katika maisha angalia watu wanataka nini halafu wape. Kama wanataka burudani wape. Kama wanataka elimu wape. Kama wanataka bidhaa wape. Kama wanataka huduma wape. Wape kwa msaada wa wataalamu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama utafiti wa mtu umevuka mipaka ya ukweli au uhalisia toa utafiti mwingine kuupinga huo wa kwake, kwa lengo la kuelimisha wengi. Haina maana kusema jambo si la kweli na usitwambie kwa nini si la kweli.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ili kupambana na matumizi mabaya ya madawa ya kulevya katika jamii ya Tanzania, ni muhimu kutoa elimu kwa Watanzania juu ya madhara yanayoambatana na matumizi ya madawa hayo. Tusipambane na madawa ya kulevya peke yake. Tupambane na elimu ya madawa ya kulevya pia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Jielimishe, usitegemee walimu kukuelimisha.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ni ya muhimu kwa sababu ya mahitaji ya lazima ya wanadamu kama vile chakula, maji, malazi, elimu, usafi, mavazi, na afya, lakini ni ya maana kwa sababu ya wanawake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Yusufu alikuwa hohehahe kabla na baada ya kuuzwa na nduguze kama mtumwa nchini Misri. Hakuwa na pesa, hakuwa na elimu, hakujuana na viongozi wa serikali. Lakini kwa vile alikuwa na Mungu, Mungu alimbariki mpaka watu wote wakashangaa. Yusufu alikuwa maskini ili mimi na wewe tuwe na tumaini leo, kwamba tukiwa na Mungu katika maisha yetu hatutatafuta utajiri. Utajiri ndiyo utakaotutafuta sisi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Pesa ina thamani pale unapokuwa nayo, si pale unapokuwa huna, hivyo iweke mahali unapoweza kuiona: katika nyumba, katika shamba au katika elimu. Badala ya kumpa mtu pesa ili ajenge nyumba, mpe nyumba. Badala ya kumpa mtu pesa ili afanye biashara, mpe biashara. Halafu, mpe elimu afanye maamuzi ya biashara yake. Pesa ina laana na Mungu pekee ndiye anayeweza kuiondoa laana hiyo. Ni rahisi kwa tajiri kupata baraka ya pesa kwa sababu ana pesa na ana uwezo mkubwa wa kusaidia maskini. Ni vigumu kwa maskini kupata baraka ya pesa kwa sababu hana au ana uwezo mdogo wa kusaidia maskini. Mungu anaweza kuondoa laana ya pesa kupitia hisani kwa maskini, kitu ambacho aghalabu hufanywa na matajiri wenye uwezo mkubwa. Heri kutoa kitu au huduma au elimu kwa maskini kuliko pesa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwaza kitu kwa dakika moja na sekunde nane – huu ni utafiti wangu tu – hicho kitu kitaanza kujiumba kwa ajili yako sehemu fulani ulimwenguni. Ukiamini kwa kiasi cha kutosha kwamba umekipata, utakipata. Haijalishi kama una elimu au huna. Hiyo ndiyo siri kubwa zaidi ya utajiri kuliko zote duniani – MAWAZO YAKO.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani lengo lake ni kutawala dunia. Huwezi kutawala dunia bila elimu!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Inavyoonekana, kadiri mtu anavyozidi kupata elimu ndivyo anavyozidi kudharau uwepo wa Shetani na uwepo wa Mungu pia. Lakini, kwa upande mwingine, ndivyo anavyoonekana hajasoma sana na ndivyo Shetani anavyozidi kulaumiwa kwa kila dhambi inayotendeka. Kuna elimu ya kidunia na kuna elimu ya kidini. Huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidunia, kwa sababu Shetani anajua ukiipata elimu hiyo hutajua kama yupo; na huwezi kutawala dunia bila elimu ya kidini, kwa sababu Mungu anajua ukiipata elimu hiyo utajua kama yupo. Hivyo, utamdharau Mungu ukipata elimu ya kidunia, utamheshimu Mungu ukipata elimu ya kidini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama Shetani anatumia elimu kutawala dunia kama vile Mungu anavyotumia elimu kutawala dunia, nani alisema kuwa baadhi ya wasanii wa ‘Bongo Movie’ na ‘Bongo Flava’ ni wanachama wa chama cha siri cha kusaidiana cha wajenzi huru? Je, wana elimu? Jibu unalo.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani ni mjanja sana. Anajua bila elimu hataweza kutawala dunia, baada ya mpango wa Mungu kukamilika. Anajua, mtu akipata elimu ni rahisi sana kujua kama Shetani hayupo. Hivyo Shetani atatimiza malengo yake bila watu kujua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Elimu ni ufunguo wa maisha lakini wengine funguo zao zina kutu!”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wengi hawana maarifa kwa sababu ya elimu na utajiri. Hawana elimu na hawana utajiri. Nchi iwape wananchi wake kila kitu isipokuwa ujinga na umaskini.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukiwa na elimu huna sababu ya kuwa maskini.”
Enock Maregesi