,

Mema Quotes

Quotes tagged as "mema" Showing 1-12 of 12
Enock Maregesi
“Hasanati ni matendo mema. Mema yanatoka kwa Mungu. Mabaya yanatoka kwa Shetani. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Mke mbaya anatoka kwa Shetani. Mke mwema ana hekima na busara, ana maadili na tabia njema, ana utu na uchapakazi, ana wema na upendo, na ana aibu kwa wanaume.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama nje ya uwezo wa kisheria ni uovu, hivyo basi, ndani ya uwezo wa kisheria ni wema. Kila mtu amepewa vipaji na Mwenyezi Mungu. Tumia vipaji vyako kutenda mema. Usitumie vipaji vyako kutenda maovu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Unabii ni uwezo alionao mtu wa kuongea mambo matakatifu ya Mungu, kuwaongoza wenzake katika njia njema. Mungu humwambia nabii kitu cha kusema na nabii huwambia wenzake kile ambacho Mungu amemwambia aseme. Mungu hawezi kuongea na watu mpaka watu wajue jinsi ya kuongea naye, na wakati mwingine ni rahisi sana kusikia ujumbe kutoka kwa mtu kuliko kuusikia ujumbe huo moja kwa moja kutoka kwa Mungu. Mungu anaweza kukwambia useme kitu fulani kwa mtu au watu fulani. Unaweza usijue kwa nini anakwambia ufanye hivyo, lakini utajisikia msukumo wa hali ya juu wa kutangaza ujumbe uliopewa kuuwasilisha. Mungu hatakulazimisha, lakini atakung’ang’aniza, na ni Mungu pekee anayejua lengo la mawasiliano hayo. Mungu akikwambia ufanye kitu fanya mara moja, usiulize kwa nini. Kazi yako ni kufanya unachotakiwa kufanya, kusema unachotakiwa kusema, si kuuliza maswali. Mtumie rafiki yako wa kiroho kukuongoza katika mema na mabaya, na usitambe – kwamba unaongea maneno uliyoambiwa na Mungu uyaongee. Ukiwa na uwezo mkubwa wa kuongea na Mungu utaleta mabadiliko katika dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Nyota ni kipaji, kipawa, takdiri, karama, au uweza; ni kiashiria cha rohoni kinachoonyesha mtu atakuwa nani baadaye, mafanikio ya mtu, au takdiri ya maisha ya mwanadamu. Unabii na nyota ya ufalme ni kibali cha Mungu katika maisha ya mtu. Kupata kibali hicho, tembea na watu sahihi katika maisha yako (tembea na watu ambao Mungu amekuchagulia kushika funguo za takdiri ya maisha yako). Tamka na kukiri kibali cha Mungu katika maisha yako yote. Panda mbegu za kibali cha Mungu katika udongo wa maisha yako. Jifunze kutenda mema bila malipo, kwani wema ni mbegu ya kibali cha Mungu. Jali mambo ya ufalme wa Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu hakutuumba ili tuwe roboti, ambayo hufanya kazi kama ilivyoelekezwa. Alituumba ili tuwe huru. Yaani, tuwe na uwezo wa kuchagua mema au mabaya – ndiyo maana akaweka Mti wa Maarifa ya Mema na Mabaya katika Bustani ya Edeni – ndiyo maana akamtuma Shetani kuwajaribu Adamu na Hawa, wazazi wetu wa kwanza.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wachawi wanaabudu miungu ambayo ndani yake kuna Shetani, aliyesababisha Ibilisi achague mabaya badala ya mema kabla Mungu hajamfukuza mbinguni. Shetani ndani yake kuna Shetani. Huyo Shetani aliyeko ndani ya Shetani, anayeitwa Roho ya Mabadiliko ya Kweli ya Ufahamu Kamili wa Siri ya Uumbaji wa Mungu (kwani ukiijua siri ya uumbaji wa Mungu unakuwa kama Mungu), ndiye anayeabudiwa na wachawi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shahidi mwaminifu na wa kweli anayajua mambo yetu yote tangu kuumbwa hadi mwisho wa dunia yetu. Kwa hiyo, ni kweli unabii lazima utimie. Mungu anataka tuwe na amani ndani ya mioyo yetu lakini anajua si jambo rahisi kwa sababu ya hila za Shetani. Shetani asingekuwepo amani ingekuwepo; watakatifu wasingekuwepo, dunia isingekuwepo. Lakini mlango wa rehema bado haujafungwa. Bado tuna uhuru wa kuchagua mema dhidi ya mabaya.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mfalme Sulemani alikuwa mtu mwenye hekima kuliko wote ulimwenguni. Anatushauri, “Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula; Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa; Maana utatia makaa ya moto kichwani pake; Na BWANA atakupa thawabu (Mithali 25:21-22). Yesu anasema jambo fulani linalofanana sana na hilo katika mafundisho Yake yaliyofuata (Mathayo 5:44-45). Kitendo cha kutukanwa, kupigwa, kushtakiwa au kulazimishwa kubeba mzigo mzito usio wa kwako kinaweza kusababisha mafutu mabaya kabisa katika asili ya binadamu. Yaani, chuki, hasira, ukatili na hata vurugu. Lakini pale wale waliobarikiwa kuwa na hekima wanapojikuta katika majaribu makubwa kama hayo tabia yao haitakiwi kuwa ya shari, inda au ya kulipiza kisasi. Bali inatakiwa kuwa ya kusaidia, kuwa na ridhaa ya kutenda mambo mema, na kuwa mwema kwa wengine siku zote.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mungu ni mtakatifu na kwa maana hiyo hatendi dhambi. Hivyo, hauwi wala hatesi. Tunajiua na kujitesa wenyewe. Ametupa hiari ya kuchagua mema au mabaya. Lakini anamtumia Shetani kama wakala wake wa kutoa adhabu kwa binadamu pale tunapoenenda sawasawa na machukizo yake. Damu ina nguvu kuliko Shetani na ina nguvu kuliko kuzimu. Unapojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani hataweza kukuona. Hivyo, hataweza kukudhuru. Lakini usipojifunika kwa damu ya Mwanakondoo, Shetani atakuona. Hivyo, atakudhuru. Atakudhuru kwa sababu Mungu atakuwa ameruhusu akudhuru, kwa sababu ya uhuru wa kuchagua mema au mabaya aliotupatia, ijapokuwa ana uwezo wa kuzuia asikudhuru. Kwa mtindo huo Mungu anakuwa ametoa adhabu kwa binadamu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukitenda mema lazima utalipwa mema, ama unajua au hujui, na ukitenda mabaya lazima utalipwa mabaya, ama unajua au hujui.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukimheshimu baba au mama yako katika mambo mema au mabaya umemheshimu Mungu katika mambo mema.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mtu akikuwaza, kwa mema au mabaya, uko moyoni.”
Enock Maregesi