,

Akili Quotes

Quotes tagged as "akili" Showing 1-25 of 25
Enock Maregesi
“Katika maisha watu wengi hawataki kukuona ukiendelea kwa sababu ukiendelea unakuwa kioo kwao. Ghafla wataanza kukutazama. Wanajua wana akili kama wewe, wamesoma kama wewe, au wana akili kuliko wewe, au wamesoma kuliko wewe, na labda wanazijua sifa zako za udhaifu na sifa zako za ushupavu toka utotoni kwako. Lakini ghafla unakuwa kioo, na wanapojitazama katika hicho kioo, wanajiona taswira zao isipokuwa sasa hawapo mahali ambapo wewe upo. Katika maisha watu watakushauri, watakufitini, watakurubuni na watakukatisha tamaa. Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona, hawajui unachokifanya na hawajui unapoelekea. Unachokiona ni takdiri ya maisha yako, unachokifanya ni kupanda mbegu na kuzimwagilia kwa imani, na unapoelekea ni kileleni. Hivyo, songa mbele, kuwa wewe daima, wape muda, wape nafasi.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Familia yako haikusaidii chochote katika mipango ya takdiri yako. Hii inasikitisha sana. Unajitahidi kila siku kuwafurahisha watu unaowapenda na watu wako wa karibu. Kila ukijitahidi kupata kibali cha watu unaishia kudharaulika na kuonekana mjinga asiyekuwa na maana. Sikiliza mazungumzo ya ndani ya moyo wako. Wapendwa wako watakukubali kama mtu hodari asiyekata tamaa, na tena watakuheshimu kutokana na tabia zako hizo. Mabadiliko haya ya kifikra hayatatokea haraka kama unavyofikiria. Yatachukua muda. Hivyo, kuwa mvumilivu. Wakati huohuo, endelea kucheza ngoma uliyoianzisha mwenyewe, endelea na mipango yako kama akili yako inavyokutuma.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Maisha tunayoishi ni mafupi, maisha ya mbinguni ni ya milele. Fundisha familia yako upendo na hofu ya Mungu, kwani hiyo ndiyo akili kushinda zote. Hekima ya kutunza familia inapatikana katika kitabu cha Mithali cha Agano la Kale.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ikiwa huna pesa na una mke na watoto kwa mfano, mke wako (wanawake walio wengi) hatakuona wa maana kwa sababu ya ustawi wa maisha ya familia yake. Ikiwa una mwanamke asiyekuwa na busara au hekima ya kutosha, au mwanamke ambaye akili zake zimefyatuka kidogo, atakusaliti kutafuta bwana au mtu mwenye maana. Kama huna pesa huna maana kwa mwanamke.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama una akili kuwa kawaida. Kama una nguvu kuwa mkarimu. Kama una pesa kuwa mnyenyekevu. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa na pesa kuwa mnyenyekevu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Potassium Cyanide si hatari inapokuwa nje. Ni hatari inapojichanganya na asidi za tumboni ambapo hubadilika na kuwa gesi ya 'hydrogen cyanide'. Gesi ya 'hydrogen cyanide' ni miongoni mwa sumu hatari zaidi ulimwenguni. Mtu akimeza kidonge cha 'cyanide' atapata madhara makubwa. Kichwa chake kitamuuma hapohapo na atachanganyikiwa akili. Ngozi yake itakuwa nyekundu, kwa sababu damu yake itakuwa nyekundu zaidi – kutokana na kuzidi kwa oksijeni katika damu. Mwili hautakuwa na uwezo tena wa kuchukua oksijeni kutoka katika damu ili uitumie, kwa hiyo damu itazidi kuwa na oksijeni zaidi. Atapumua kwa shida. Mapafu yake yatafanya kazi vizuri lakini mwili wake hautakuwa na uwezo wa kutumia oksijeni yoyote – hivyo atadhani ana matatizo katika mfumo wake wa kupumua. Atazimia. Yaani, oksijeni haitafika kwenye ubongo. Atapata kifafa na atatapika nyongo. Ubongo wake utashindwa kufanya kazi na atakuwa mahututi ndani ya sekunde kumi! Baada ya hapo moyo wake utasimama kufanya kazi, na atafariki dunia.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Hii ni sheria ya akili yangu: Akili yangu ni muhimu kuliko familia yangu. Nisipoitunza vizuri akili yangu, sitaitunza vizuri familia yangu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Akili yako isipokuwa timamu, familia itakushinda. Familia ikikushinda utalaumiwa na Mwenyezi Mungu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“If you are smart be simple. If you are powerful be generous. If you are rich be humble. If you want to be smart be simple. If you want to be powerful be generous. If you want to be rich be humble.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kila mtu ana tabia, matendo, mawazo na akili yake tofauti na mtu mwingine hapa duniani. Usimdharau mtu ukidhani ana akili kama za kwako au anafikiri kama unavyofikiri wewe kwani kila mtu aliumbwa kivyake na Mwenyezi Mungu. Unaweza kudhani unamjua mtu kumbe humjui. Heshimu kila mtu kama unavyojiheshimu kwa sababu, kila mtu ni wa pekee. Kama tunavyotofautiana katika vidole na macho ndivyo tunavyotofautiana katika tabia, matendo, mawazo, imani, maadili na akili. Usimdharau mtu usiyemjua au unayedhani unamjua.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Watu wa zamani katika Agano la Kale walikuwa wakiabudu miungu iliyotengenezwa kwa mawe na vinyago. Miungu hiyo haikuwa na chochote ndani mbali na kutengenezwa kwa akili na fikira za kibinadamu. Hii ilikuwa ni kinyume cha ukweli wa Kibiblia kwamba Mungu alimuumba mtu kwa mfano wake, lakini si mtu aliyejaa dhambi kumtengeneza Mungu kwa mfano wake. Kuabudu miungu mingine ni dhambi kubwa. Tii Amri Kumi za Mungu; hasa ya kwanza, ya pili na ya tatu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Shetani hawezi kusoma ndani ya mioyo ya wanadamu mpaka wanadamu wenyewe wamwonyeshe. Ukionyesha tamaa ya ngono, Shetani atakupa ngono. Ukionyesha tamaa ya ulevi, Shetani atakupa ulevi. Ukionyesha tamaa ya wizi, Shetani atakupa wizi. Ukionyesha tamaa ya chuki, Shetani atakupa chuki. Ukionyesha tamaa ya upendo, Mungu atakupa upendo. Kama kuna ubishi kati ya moyo wako na akili yako, fuata moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Lakini kuna ndoto takatifu na kuna ndoto za kishetani. Ndoto takatifu hutokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika, kama ambavyo usiku unavyokuwa kimya na kila kitu kimetulia, karibu na saa za alfajiri, ambapo mfumo wa usagaji chakula unakuwa umemaliza kazi yake. Kipindi hicho malaika wa Mungu hutufunulia siri kuhusu ulimwengu huu, ili kwamba tutakapoamka asubuhi tuwe na baadhi ya maarifa yaliyojificha ndani ya maandiko ya vitabu vitakatifu; kwa sababu malaika wa Mungu ndiye anayetawala ufahamu wetu, kama ambavyo Mungu anavyotawala hiari yetu, na kama ambavyo nyota zinavyotawala miili yetu. Lakini kwa wale waliokomaa kiimani malaika mwema anaweza kuwafunulia siri wakati wowote, haijalishi wamelala au wameamka. Kwa ajili ya ujanja wa Shetani ndiyo maana Mungu hutufunulia siri zake, ili tujihadhari naye.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama una akili, kama una uwezo wa kuota ndoto, na kama wewe ni mchapakazi hodari, hakuna kitakachoshindikana.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kama ulikuwa ukimwambia mwanao kuwa atakuwa jambazi labda kwa sababu ya fujo zake alipokuwa mdogo, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota atakapopevuka akili ni ya kihalifu. Kwani hayo ndiyo mambo ya kwanza kabisa kujirekodi katika ubongo wake alipokuwa hajitambui. Lakini kama ulikuwa ukimwambia kuwa atakuwa daktari au mwanasheria, mambo mengi atakayokuwa anayafikiria au anayaota ni ya kidaktari au kisheria. Kuna uwezekano mkubwa akawa daktari au mwanasheria baadaye katika maisha yake.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Akili ya mipango ni bora kuliko akili ya darasani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Wanasayansi wanasema hakuna Mungu kwa sababu hawawezi kumwona wala kumgusa. Lakini nao hawana akili kwa sababu hawawezi kuiona wala kuigusa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haibabaishwi na huruma. Inababaishwa na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haishirikiani na huruma katika kufanya maamuzi yake. Inashirikiana na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Serikali haiendeshwi na huruma. Inaendeshwa na akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ufalme wa mbinguni uko juu. Akili ya binadamu iko juu. Kupata Amri Kumi za Mungu, Musa alipanda juu katika mlima Sinai. Yesu alijaribiwa na Shetani akiwa juu katika jangwa la Yuda. Ukifanikiwa tunasema uko juu. Tai hawezi kuona vizuri akiwa chini anaweza kuona vizuri akiwa juu. Ulaya na Amerika tunaita majuu kwa sababu ziko juu ya ikweta. Kwa nini juu? Kwa sababu juu kuna utukufu.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ukipata shida itakupa akili ya kufanikiwa, kwani shida ni kipimo cha akili.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“ATP inaweza kukusaidia kupata akili na nguvu ya kufanya jambo ambalo katika hali ya kawaida lisingewezekana. Wakati mwingine unaweza kufanya jambo hata wewe mwenyewe ukashangaa umelifanyaje. Unaweza kwa mfano kufukuzwa na mnyama mkali ukapenya mahali ambapo, katika hali ya kawaida usingepenya. Sasa usishangae tena. Kilichofanya upenye ni ATP.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Akili ya peke yako haina maana. 2 + 2 = 5.”
Enock Maregesi