,

Maono Quotes

Quotes tagged as "maono" Showing 1-6 of 6
Enock Maregesi
“Kitabu cha KOLONIA SANTITA kinaweza kusomwa na watu wenye umri wa kuanzia miaka 13 na kuendelea. Katika umri wa miaka 13 fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali. Watoto katika umri huu wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia, na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na uhakika, kama nadharia ya KOLONIA SANTITA.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kuna ndoto za mchana na kuna ndoto za usiku. Ndoto za mchana ni maono ya kile ambacho roho inatamani kuwa. Ndoto za usiku ni maono yanayotokea wakati akili imetulia baada ya mwili wote kupumzika. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira; ukiota kuhusu maji, hiyo ni ishara ya siri; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni; ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio. Kitu cha kwanza kufanya unapoota ndoto za kishetani, utakapoamka, mwombe Mungu akunusuru kutoka katika matatizo yoyote yanayokunyemelea; au yanayomnyemelea mtu mwingine yoyote yule, hata usiyemjua. Ubongo ni kitu cha ajabu kuliko vyote ulimwenguni na umetengenezwa na Mungu. Ndoto zinapatikana ndani ya ubongo. Ubongo unapatikana ndani ya ufahamu. Ufahamu mtawala wake ni malaika mwema. Malaika mwema anajua siri ya ndoto. Kila mtu anaota na kila ndoto ina maana yake. Rekodi ndoto zako kila siku kwa angalau mwezi mzima kupata maana halisi ya ndoto hizo, na kujua kwa nini ulizaliwa.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Ndoto za wachawi ni tofauti kidogo na ndoto takatifu. Wachawi wanapokuwa hawahitaji kusafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini wana hamu ya kuona wenzao wanafanya nini au wanasema nini, huwa wanalala ubavu mmoja upande wa kushoto kwa jina la mungu wao na la mashetani wote. Kisha wanatoa mvuke wa bluu midomoni mwao. Kupitia mvuke huo, kwa nguvu za Shetani na kwa ruhusa ya Mwenyezi Mungu, wataona na watasikia kila kinachofanyika upande wa pili. Kile wanachotaka kukiona na kukisikia hujifunua katika ufahamu wao kama taswira au maono, kutoka katika akili isiyotambua, ya watu wakifanya au wakisema kitu. Kama wanataka kujua siri za watu wengine, hata wale ambao si wachawi, watazijua kupitia ndoto hizo; kwa sababu ya makubaliano ya wazi, si ya siri, waliyoingia na Shetani. Makubaliano hayo si ya lelemama; yaani yale ambayo hufanywa kwa kutoa kafara ya mnyama, au kufuru ya aina yoyote ile kwa Mwenyezi Mungu, au kwa kuabudu dini za kichawi. Lakini ni kwa sadaka halisi ya wao wenyewe ya mwili na roho kwa Shetani na kwa kufuru ya kuikana kabisa, imani ya Mwenyezi Mungu. Lakini hiyo ni kwa wale wanaotumia uchawi wa kishetani. Wale wanaotumia uchawi wa asili, kama vile kutumia risasi kumroga mtu kwa sababu risasi mungu wake ni sayari ya Zohali, au wale walioingia mkataba wa siri na Shetani, hawana uwezo wa kuota hivyo. Hivyo, si kila mchawi anaweza kuota ndoto za namna hiyo, ni kwa wale tu walioingia mkataba wa wazi na Shetani.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Kujua nini kitatokea kesho, au kesho kutwa, au kujua jinsi usaili wako wa kazi utakavyokuwa, au ni maswali gani utakayoulizwa kwenye mtihani kwa mfano, kutarahisisha sana maisha yetu. 'Madirisha' madogo katika kipindi cha saa za usoni hufunguka mara kwa mara katika maisha yetu, kimiujiza na bila kutegemea. Hudokeza kidogo jinsi tukio fulani, au hali fulani, au kitu fulani kitakavyotokea katika kipindi cha wakati ujao bila sisi wenyewe kujua. Hali hii hujulikana kama jakamoyo. Jakamoyo ni sanaa ya kubashiri vitu visivyojulikana. Kazi yake ni kutuhadharisha na kutusaidia! Kujua mapema hatari iliyoko mbele yako inamaanisha kuwa na uwezo wa kujilinda kutokana na hatari hiyo, na kuwa na uwezo wa kuepuka mitego. Jakamoyo huweza kumtokea mtu katika hali ya 'maono', au 'mwako wa mwanga' (yaani kufumba na kufumbua). Mara nyingi huonekana kama ndoto. Hutokea wakati mtu amelala usingizi. Ikitokea wakati mtu yuko macho, wakati mwingine huendana na misisimko ya mwili kabla ya mwako, ikiwa na maana ya kumfanya mtu awe makini na kitu chochote kinachotarajia kutokea. Ndiyo maana baadhi ya watu utakuta wakisema wanaumwa tumbo, kifua au kichwa cha ghafla katika kipindi ambacho taswira ya tukio fulani inakuwa ikitokea akilini mwao, ikiwaambia waende mahali fulani bila kukosa kwa mfano, na kadhalika. Hakuna mtu anaweza kufanya jakamoyo imtokee. Hutokea yenyewe muda wowote kuleta ujumbe, kuhusiana na matukio ya wakati ujao. Kamwe usipuuze wito wa moyo wako.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Aidha, tunaweza kupata inkishafi kutokana na asili ya miili yetu, matukio fulani ya wakati ujao yana asili yake katika ndoto za binadamu. Ndoto hizo au maono hayo ni ishara ya kile kinachokuja mbele katika maisha ya mtu; kama vile afya, ugonjwa au hatari. Ukiota kuhusu moto, hiyo ni ishara ya hasira – unatakiwa kuwa na hekima; ukiota kuhusu mimba na unajifungua, hiyo ni ishara ya kuwa katika mchakato wa kutengeneza wazo jipya – unatakiwa kushukuru; ukiota unaruka angani, hiyo ni ishara ya tumaini – unatakiwa kushukuru; ukiota kuhusu maji au kiowevu kingine chochote kile, hiyo ni ishara ya siri na wakati mwingine ni ishara ya kuwa na matatizo ya kiafya kama utaota kuhusu maji machafu – unatakiwa kuwa msiri na msafi; ukiota kuhusu ardhi, hiyo ni ishara ya huzuni – unatakiwa kuomba; na ukiota kuhusu Yesu, hiyo ni ishara ya mafanikio – unatakiwa kushukuru.”
Enock Maregesi

Enock Maregesi
“Mfundishe mtoto wako maadili mema kwa miaka kumi na tatu, katika umri wa miaka kumi na tatu fikra za mtoto huanza kuwa na maono na utambuzi wa vitu mbalimbali na watoto katika umri huo wanao uwezo wa kuchambua dhana kadha wa kadha za kinadharia na hali kadhalika wanao uwezo wa kuchambua nadharia tata zisizokuwa na hakika na hata zile zenye hakika zisizokuwa tata, kabla hujamkabidhi kwa dunia. Ukimkabidhi mtoto wako kwa dunia kabla ya umri wa miaka kumi na tatu, kama vile kumpeleka katika shule ya bweni au kumpeleka akalelewe na watu wengine ambao si wazazi wake, yale ambayo hukumfundisha atafundishwa na ulimwengu. Mpeleke mtoto wako katika shule ya bweni au kuishi na watu wengine akiwa amefundishwa maadili mema. Kinyume cha hapo atafundishwa na shule au watu wengine kwa kudharauliwa, kuchukiwa na kuadabishwa.”
Enock Maregesi